Tuesday, July 16, 2013

TANZANIA YATAKA SHERIA ZA WALINDA AMANI KUBADILISHWA

Tanzania inapendekeza kufanyiwa, marekebisho sheria ya kulinda amani, kuwezesha vikosi vya kulinda amani kujikinga na mashambulizi. Hii ni baada ya walinda amani saba wa Tanzania kuuawa na watu waliokuwa wamejihami eneo la Darfur mwishoni wa wiki.Wanajeshi wengi walijeruhiwa baadhi wako mahututi. Mauaji ya walinda amani 7 wa Tanzania nchini Sudan imewashangaza wengi sana nchini humo kulingana na naibu waziri mkuu kwani nchi hiyo ndio imeanza kushika kasi katika juhudi zake za amani kimataifa. .
Maafisa hawakuwa na taarifa kamili kuhusu uvamizi wa Jumamosi ambapo wanajeshi wengine 14 walijeruhiwa vibaya katika shambulizi baya zaidi kushuhudiwa dhidi ya vikosi vya kimataifa nchini Sudan.
Shambulizi hilo lililofanywa na kikundi kikubwa cha watu waliokuwa wamejihami, lilihusisha mashambulizi makali ya mizinga na iliyolenga wanajeshi hao umbali wa kilomita 25 Magharibi mwa mji wa Khor Abeche.
Tanzania, ambayo pakubwa ni nchi salama na thabiti katika Kanda ya Afrika Mashariki, imeendelea kujitolea sana katika juhudi za amani duniani. Mwaka jana ilikuwa nchi ya kwanza kujitolea kupeleka vikosi vyake Mashariki mwa Congo, chini ya kile ambacho kitakuwa kikosi cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa wenye jukumu la kupambana vilivyo na makundi ya waasi huko.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO