Wednesday, July 03, 2013

UAE YAWAFUNGWA WATU 61 KWA NJAMA ZA MAPINDUZI

Watu 61 waliopatikana na hatia ya kula njama ya kufanya mapinduzi wamehukumiwa vifungo vya hadi miaka 10 gerezani leo hii katika Umoja wa Falme za Kiarabu kufuatia kesi iliowalenga Waislamu wa itikadi kali na kushutumiwa na makundi ya haki za binaadamu.
Miongoni mwa waliohukumiwa ni wanataaluma, wanasheria na ndugu wa familia mashuhuri za Umoja wa Falme za Kiarabu akiwemo binamu wa mtawala wa mojawapo ya falme saba zinazounda umoja huo wenye utajiri wa mafuta ambao ni adui wa muda mrefu wa makundi ya Kiislamu yanayotaka kuwa na usemi katika masuala ya kisiasa na ya kitaifa katika umoja huo.
Mahakama Kuu ya nchi hiyo imewahakumu watu wanane kati yao hao kifungo cha miaka 15 gerezani bila ya wenyewe kuweko mahakamani. Serikali imesema hukumu hizo haziwezi kukatiwa rufaa. Shirika la haki za binaadamu la Human Rights Watch limesema hukumu hizo zinaonyesha kuzidi kuwa mbaya kwa rekodi ya haki za binaadamu ya Umoja wa Falme za Kiarabu wakati kundi la haki za binaadamu lilioko Uswisi la Alkarama limesema hukumu hizo zimechochewa kisiasa na limetaka zibatilishwe.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO