Mfanyakazi wa zamani wa shirika la ujasusi la Marekani, Edward Snowden, ameomba hifadhi ya ukimbizi nchini Urusi, huku mataifa ya Ulaya yakitaka majibu juu ya ripoti kwamba Marekani ilikuwa ikiwapeleleza maafisa wa Umoja wa Ulaya. Ripoti hiyo iliyochapishwa na jarida la Der Spiegel la hapa Ujerumani, ilitotokana na taarifa za karibuni kabisa kuvujishwa na Snowden. Mmarekani huyo amekuwa akipiga kambi nje ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Moscow zaidi ya wiki moja sasa, akiepuka kusafirishwa kupelekwa kwao, anakokabiliwa na mashitaka ya kula njama dhidi ya nchi yake. Hapo jana, Rais Vladimir Putin alimpa Snowden sharti awache kuvujisha taarifa za kijasusi. Snowden ameutuhumu utawala wa Rais Obama kujaribu kumzuia kutumia haki yake ya kuomba hifadhi. Katika taarifa yake kwa mtandao wa WikiLeaks, alisema Rais Barack Obama alimuamuru Makamu wake, Joe Biden, kuzishinikiza nchi alizoomba hifadhi, zimkatalie.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO