Madereva
wa mabasi mjini New York, Marekani, wameendelea na mgomo wao kwa siku ya pili
mfululizo. Madereva hao wameendelea na mgomo huo kulalamikia ukosefu wa usalama
wa shughuli yao hiyo. Kufuatia mgomo huo, wazazi wamejikuta katika wakati
mgumu, kutokana na kushindwa kuwapeleka watoto wao mashuleni. Taarifa zinasema
kuwa, Meya wa mji New York Michael Bloomberg amesema kwamba, suala la kuweka
usalama katika shughuli za madereva wa mabasi katika mji huo ni jambo
lisilowezekana. Mgomo huo unafanyika katika hali ambayo siku kadhaa zilizopita
mazungumzo kati ya viongozi wa mji wa New York na muungano wa chama cha
madereva wa mabasi ya shule nchini Marekani, yalishindwa kufikia mwafaka
kuhusiana na kuwepo kwa kiwango cha chini cha hali ya usalama katika shughuli
za madereva hao. Muungano huo wa chama cha madereva mjini New York umesema
kuwa, kuna uwezekano mkubwa kwa madereva hao kuacha kazi zao baada ya
kumalizika kipindi cha mkataba wao mwezi Juni mwaka huu. Mauaji ya kiholela kwa
kutumia silaha moto ni jambo la kawaida katika mitaa ya Marekani. Mara kwa mara
kumekuwa kiripotiwa mauaji ya umati yakifanyika kwenye maeneo mbalimbali hasa
mashuleni huko Marekani.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO