Chama kikuu cha kisiasa nchini Mali kimetoa wito leo wa kufanyika mkutano haraka wa wagombea urais waliojitiokeza baada ya mkuu wa tume ya uchaguzi kueleza wasiwasi wake kuwa uchaguzi uliopangwa kufanyika mwezi huu hautakuwa huru na wa haki. Rais wa mpito wa muungano wa kidemokrasia nchini Mali Iba Ndiaye amesema kuwa kutokana na changamoto zinazofahamika ambazo zinakutikana katika mchakato wa kuelekea uchaguzi, serikali inapaswa kuitisha kikao cha wagombea urais pamoja na vyama vya kisiasa kuangalia sheria na kuepuka mivutano ya baada ya uchaguzi vyama na wagombea kupinga matokeo.
Mamadou Diamoutani, afisa wa ngazi ya juu wa tume ya uchaguzi ya taifa hilo la Afrika magharibi , amesema kuwa mapungufu kadha katika mchakato huo wa uchaguzi unaweza kusababisha matokeo ya uchaguzi wa hapo Julai 28 kupingwa.
Mali inajitayarisha na uchaguzi baada ya kushuhudia mapinduzi mwaka jana pamoja na mapigano ya waasi wa Kiislamu. Umoja wa Mataifa umezindua kikosi cha kulinda amani siku ya Jumatatu ili kuiruhusu Ufaransa kuondoa majeshi yake ambayo yalikuwa yakiisaidia serikali ya mpito kulinda amani.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO