Thursday, February 02, 2012

NAAGA NDUGU NAAGA

Ya Allah Karimu, Mmiliki wa Uhai,
Nimeshika kalamu, Nafurahi nipo hai,
Leo imeniladhimu, Niage ningali hai,
Forodhani:Unguja,Buriani ikhwani.

Siku yangu ikifika, Kauli itakapo funga,
Siku yangu ikifika, Kauli itakapo funga,
Kifo kweli natamka, Jamani hakina kinga,
Oman: Uamarika, Buriani ikhwani.

Siku imefichikana, Anayejua manani,
Usiku au Mchana, Sitambui abadani,
Nafsii ya kuagana, Ameridhia manani,
Pemba Yemen Londona, buriani ikhwani.

Kama nikifa porini, Niwe mlo wa wanyama,
Au kule baharini,Samaki wanile nyama,
Mema ya mtu thamani, Roho yaishi salama,
Canada,Bahraini,Buriani ikhiwani.

Kikinifika nyumbani,Niosheni ndugu yenu,
Na sanda nivisheni, Nadua zitoke kwenu,
Kaburini ni wekeni,Fikirini zamu yenu,
Belgium Udachini, Buriani Ikhiwani.

Wale nilowakosea,Nisameheni Jamani,
Haikuwa yangu nia, Adui yetu Shetani,
Mimi walonikosea, Sina kinyongo Moyoni.
German na Romania,Buriani ikhiwani.

Beti Saba nimefika, Nami nenda Msibani,
Taarifa imefika, Amefariki jirani,
Kifo ninakikumbuka, Na mimi nipo njiani,
Waislamu Wenzanguu, Naaga ningali hai


by;Becker Salim Omar, Master Hassan and Maalim Moussa Kijangwa.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO