Thursday, October 25, 2012

BARAZA LA EID TANZANIA

JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAM TANZANIA INAWAALIKA WAISLAM WOTE BARAZA LA IDD KESHO IJUMAA BAADA YA SALATUL JUM'A KATIKA MSIKITI WA MTAMBANI.

 MASHEIKH MBALI MBALI WATATOA MADA MBALI MBALI NA KUTOA TAMKO DHIDI YA DHULMA DHID YA WAISLAM ZINAZOENDELEA NCHINI TANZANIA.


Thursday, October 18, 2012

Assalaamu 'alaykum warahmatullaahi wabarakaatuh. 



YALIYOJILI MAHAKAMANI KWA SIKU YA LEO KUHUSIANA NA HABARI ZA SHAIKH PONDA NA WAISLAMU WOTE WALIOKAMATWA MBAGALA.

 Kutokana na mahojiano ya jana ya shaikh ponda aliachwa na kesi 2 ambazo bado hakuhojiwa ikiwa ni ya kidongo chekundu pamoja na sakata la Markaz chang'ombe.lkn cha ajabu leo hii amehojiwa swala la markaz tuu kisha kupelekwa mahakamani. Kitu kingine cha kushangaza ni kwamba kesi zote 4 alizosomewa kwamba zinamkabili hazikusikilizwa na wameshikilia habari ya markaz. Lkn kesi imehairishwa mpaka itakaposikilizwa tena tarehe 1 november kutokana na hakimu aliyekuwepo kusema hiyo kesi haishikilii yeye kwa hiyo asubiriwe hakimu aliyepangiwa hiyo kesi kwa ajili ya kutoa hukumu ya ponda pamoja na waislamu wengine 49 wanaoshikiliwa na polisi. Wakili wa shaikh ponda alipotaka dhamana akaambiwa kama ifuatavyo : vijana hao 49 dhamana itatolewa lkn si kwa wakati huu kwa vile bado haikupangwa, na hata wakipata dhamana itakuwa kwa masharti makali na magumu sana. Kwa upande wa Ponda ni kwamba hakuna kitu kinachitwa dhamana kwake yeye kwani ni maagizo kutoka kwa DPL. Wakili alipohoji kwa nini dhamana kwa upande wa ponda isiwepo akajibiwa ni kwa sababu ya usalama wa Taifa la Tanzania. Lakini wakili akataka ajue ni usalama gani ambao unahofiwa ponda akiwa nje ? Hakimu hakujibu chochote bali akamwambia hiyo ni taratibu iliyopangwa na sharia na usitake kujua zaidi, na kama unataka dhamana basi asubiriwe huyo hakimu aliyepangiwa hiyo kesi hadi atakapoisikiliza tarehe 1 november.



 WITO KWA WAISLAMU 



KUTOKANA na kunyimwa dhamana kwa shaikh ponda na waislamu wengine 49 waislamu wote wametakiwa kwa siku ya kesho ijumaa insha allah kuitumia vizuri ili kuhakikisha kwamba kama wanasheria hawakuona kipengele cha dhamana kwa sababu ya usalama wa Taifa,kuhakikisha wanawaonesha wanasheria kipengele cha dhamana kwa kutumia qur'an.Hivyo waislamu wote wa Dar es salaam tunatakiwa kwa swala ya Ijumaa ya kesho insha allah kuswalia misikiti ya mjini na baada ya hapo kuwaonesha wanasheria sehemu ya dhamana kama wao hawajaiona.So waislamu tujiandae kwani mkae mkijua kwamba ijumaa ya kesho kutakuwa hapatoshi Dar es salaam. HAYO YOTE YAMETOLEWA NA SHAIKH MAPEO PINDI WALIPOTOKEA MAHAKAMANI BAADA YA SWALA YA AL'ASWRI HII KTK MSIKITI WA MTAMBANI K/NDONI DAR ES SALAAM.




 PIA UMETANGAZWA UONGOZI AMBAO ULITEULIWA NA KIKAO CHA JANA BAADA YA SHURA YA MAIMAMU WA DAR ES SALAAM NI KAMA IFUATAVYO. 1.AMIR NI SHAIKH MAPEO AKISAIDIWA NA SHAIKH KONDO BUNGO. 2.ANAYESHIKA NAFASI YA SHAIKH PONDA NI OST. JAFFAR. NB: IDHAA MAATA SAYYIDU QAAMA SAYYIDU { PINDI ANAPOKUFA KIONGOZI ANASIMAMA KIONGOZI } CHA MUHIMU SAMI'INAAA WA-ATWA'ANAA.


 ASSALAAMU 'ALAYKUM WARAHMATULLAAHI WABARAKAATUH.







Wednesday, October 17, 2012

KUKAMATWA KWA SHEIKH ISSA PONDA.

TAARIFA YA DHARURA 
Asalaam Alaykum! 
Saa 4 asubuhi nilifika Central Police 
kusimamia mahojiano yake na Polisi kwa mujibu wa haki za mtuhumiwa nilionana na msaidizi wa ZCO daada ya utambulisho na kumfahamisha haki zake wakati wa mahojiano alihojiwa. Ukiacha namna alivyokamatwa mpaka naondoka polisi saa 10 kasoro alikuwa ktk hali nzuri na polisi akiwa kituoni
hawakumfanyia lolote lililokinyume na haki za mtu aliyechini ya ulinzi. 
Sheikh anatuhumiwa na mambo yafuatayo:
- 1. Kuhamasisha maandamano kwenda Wizara ya Mambo ya Ndani. Wakati wa mahojiano walitaka kujua yafuatayo:-
                  i. kwanini waliandamana
                 ii. nani aliandaa mabango
                iii. kwanini walisema kuwa baada ya maandamano yale wataenda    

                     kumng'oa Mufti na Ndalichako

                iv. nani aliandaa maandamano Sheikh alikiri kuhamasisha 

                    maandamano na pia alikubali ujumbe uliuokuwa katika mabango 

                    ulikuwa umebeba hisia za waislamu. Isipokuwa yeye hajui nani 
                    aliyaandika hayo mabango.

 Kuhusu Mufti na Ndalichako alisema wanastahili kuondolewa kwasababu ya kuongoza kwa dhulma dhidi ya waislamu. Pia alisema maandamano yaliandaliwa na Taasisi na Jumuiya za Kiislamu na yeye ni katibu wake.

 2. Kuvamia kiwanja cha chang'ombe Hapa alijibu kuwa huo ni mgogoro wa ardhi na waislamu wapo pale kwasababu ni kiwanja cha waislamu. Na kama kuna mtu anadai amevamiwa eneo lake huo ni mgogoro wa ardhi
aende kushitaki mahakama ya ardhi na waislamu wapo tayari kufika mahakamani kujibu. Pia alikiri kuwa amehusika ktk ujenzi wa msikiti unaojengwa ktk eneo hilo.

 3. Kuhamasisha maandamano kidongo chekundu 
 
4. Vurugu mbagala. Haya mawili ya mwisho hakuhojiwa kwasababu mafaili yanayohusu malalamiko hayo yalikuwa hayajafika central lakini vilevile muda ulikuwa umeenda sana. Kwani mpaka tunamaliza mahojiano ilikuwa ni saa kumi kasoro hivi toka saa nne asubuhi. DHAMANA. Baada ya mahojiano niliomba apatiwe dhamana na kesho afike polisi kwa mahojiano zaidi. Polisi waliokuwa wanamhoji walikataa kwa hoja kuwa suala hilo liko kwa viongozi wakuu wa jeshi la polisi. Waliomba nikamwone ZCO Bw. Msangi, yeye alisema hawezi kulitolea maamuzi akanitaka nimwone Kamanda Kova. Nilienda kuonana na Kamanda Kova naye aliniambia kuwa hawawezi kutoa dhamana mpaka amalize mahojiano yaliyobaki. Na vile vile alisema wanasubiri wapate ushauri toka ofisi ya DPP. Lakini zaidi akasema kwa kuwa issue ya mbagala kuna watu wameshitakiwa kwa armed robbery kosa ambalo halina dhamana si vizuri kumpa dhamana sasa kwani huenda katika upelelezi wao wanaweza kumuunganisha na washitakiwa wa armed robbery mbagala. Kwa ufupi hiyo ndio hali iliyokuwepo. 


NAOMBA WAISLAMU WAAMBIWE WAWE NA SUBIRA WAKATI HUU WAIFANYE LOLOTE LITAKALOWAPA NAFASI MAADUI WA UISLAMU MANENO YA KUSEMA Maasalamu!
By Brother Juma Nassoro - Wakili





















DHUL-HIJJAH

Assalam alaykum warahmatul lahi wabarakatu.Amma baada ya kumshukuru Mwenyezimungu na kumtakia Rehma na Amani Mtume wa Allah na kipenzi chetu mtume Muhammad swallal lahu alayhi wasallam. MSAMU kwa ushirikiano na jumuiya nyingine za kidini inapenda kuwatangazia rasmi kuwa JUMATANO ya Tarehe 17 Oktoba ndio siku ya kwanza ya Dhul- Hijjah na Arafa itakuwa ni siku ya Alkhamis sawa na tarehe 25 Oktoba 2012 na Iydul-Adhw-haa itakuwa ni siku ya Ijumaa tarehe 10 Dhul-Hijjah sawana Oktoba 26.




Pia tunapenda kuwakumbusha ndugu zetu wengi jambo ambalo wanaghafilika nalo, kuwa, wenye kunuia kuchinja au kuchinjiwa, kuanzia unapoingia tu mwezi wa Dhul-Hijjah wanatakiwa wajizuie kukata nywele na kucha mpaka watakapomaliza kuchinja. Haya ni maamrisho yanayopatikana katika Hadiyth ifuatayo:


عن أم سلمة رضي الله عنها، أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: ((إذا رأيتم هلال ذي الحجة وأراد أحدكـم أن يضحّي فليمسك عــن شعره وأظفاره) وفي راوية: ((فلا يأخذ من شعره ولا من أظفـاره حتى يضحّي)) مسلم


Imetoka kwa Ummu Salamah (Radhiya Allaahu 'anha) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Ukiandama mwezi wa Dhul-Hijjah na ikiwa yuko anayetaka kuchinja basi azuie (asikate) nywele zake na kucha zake)
Na katika riwaya nyingine ((Asikate nywele wala kucha mpaka akimaliza kuchinja))[Muslim na wengineo]. 




Siku Kumi Bora Kabisa Za Allah


Inatupasa tumshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kwa neema Aliyotujaalia ya kutuwekea miezi mitukufu, au siku tukufu au nyakati tukufu ambazo vitendo vyake vyema huwa na thawabu nyingi sana. Na hivi tunakaribia kabisa kuingia katika mwezi mwingine mtukufu wa Dhul-Hijjah. Katika mwezi huu, siku kumi za mwanzo ni siku bora kabisa katika dunia na zina fadhila kubwa kutokana na dalili zifuatazo:


عن ابن عباس رضي الله عنهما، أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: ((ما من أيام العمل الصالح فيها أحب إلى الله من هذه الأيام)) - يعني أيام العشر-. قالوا: يا رسول الله، ولا الجهاد في سبيل الله ؟ قال: ((ولا الجهاد في سبيل الله، إلا رجل خرج بنفسه وماله ثم لم يرجع من ذلك بشيء)) البخاري

Imetoka kwa Ibn Abbaas (Radhiya Allaahu 'anhuma) kwamba Mjumbe wa Allaah amesema: ((Hakuna siku ambazo vitendo vyake vyema Anavipenda Allaah kama siku kumi hizi)) (siku kumi za mwanzo wa mwezi wa Dhul-Hijjah) Akaulizwa, je, hata Jihaad katika njia ya Allaah? Akajibu (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ((Hata Jihaad katika njia ya Allaah isipokuwa mtu aliyekwenda na nafsi yake na mali yake ikawa hakurudi na kimojawapo)) [Al-Bukhaariy].


Miongoni mwa ubora wake ni:

1.Amali Zake Ni Bora Kuliko Kwenda Katika Jihaad Fiy SabiliLLaah

Monday, October 01, 2012


YAJUE MAKOSA MBALIMBALI YAFANYIKAYO KATIKA IBADA YA HIJJA

IHRAMU NA MAKOSA YAKE

Imethibiti katika Sahihul Bukhari na Muslimu kuwa Mtume (Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallama) amewapangia waislamu wa sehemu na pembe mbalimbali za dunia sehemu zao za kuhirimia wanapotaka kufanya ibada ya Hijja au Umrah. Sehemu hizo ni kama zifuatazo:

1. Dhul Hulayfah kwa watu wa Madiynah

2. Juh’fa kwa watu watokao Shamu

3. Qarnul Manaazil kwa watu wa Najd

4. Yalamlam kwa watu watokao Yemen

baadhi ya Mahujaji wanaokwenda moja kwa moja Makkah badala ya kuhirimia katika sehemu hizo wakiwa katika ndege au katika usafiri wowote walionao na si kusubiri hadi wateremke uwanja wa ndege wa Jiddah ndipo wahirimie. Haya ni makosa na ni kukhaalifu amri ya Mtume (Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallama).

MAKOSA YA KIVITENDO YANAYOAMBATANA NA KUTUFU AU KUZUNGUKA AL-KA’ABAH

1.Kuanza kuzunguka Al-Ka’abah kabla ya kufika sehemu ya jiwe jeusi, na kwa sasa kuna alama ya mstari maalumu inayoonyesha lilipo jiwe jeusi na kama ni usiku kuna taa ya rangi maalumu taa ya kijani yenye kuonyesha lilipo jiwe jeusi.

2.       Kutufu ndani ya eneo linaloitwa Hijr kutokana na msongamano mkubwa wa watu. Kimsingi hili ni kosa kubwa kwa kuwa eneo la Hijr kishari’ah liko ndani ya Al-Ka’abah na tawafu inatakiwa iwe nje ya Al-Ka’abah na sio ndani ya Al-Ka’abah. Kwa hiyo kwa kupita ndani ya Hijr unapotufu unakuwa umetufu katika sehemu ya Al-Ka’abah na si Al-Ka’abah yote ambayo ndiyo inayotakiwa.

3.   Kukimbia kimbia katika Tawafu zote saba.

4.      Kusongamana na kupigana vikumbo kwa ajili ya kulifikia jiwe jeusi ili kulibusu, jambo ambalo mara nyingine husababisha watu kurushiana matusi na hata kupigana na kwa kufanya hivyo wakawa wanaivunjia heshima nyumba tukufu ya Allaah. Kutufu kwa namna hii kunapunguza daraja ya kutufu bali mara nyingine hata kuipunguza tija ibada nzima ya Hijja

5.      Itikadi ya baadhi ya Mahujaji kuwa jiwe jeusi linanufaisha au linadhuru kwa dhati yake hivyo utawakuta pindi wanapoliamkua wanajipangusa katika viwiliwili vyao au wanawapangusa watoto wao walionao katika ibada ya Hijja au ‘Umrah. Na yote haya ni kutokana na ujinga na ni upotevu wa wazi.

6.      Baadhi ya Mahujaji kung’ang’ania nguzo zote za Al-Ka’abah na mara nyingine wakawa wanazishika kuta zote za Al-Ka’abah na hata mara nyingine kuing’ang’ania sana Al-Ka’abah kwa kila sehemu au wakawa kila wakiigusa Al-Ka’abah wakawa wanajipangusia. Na huu ni ujinga na upotevu wa wazi.

 

MAKOSA YA KUSIMAMA KATIKA VIWANJA VYA ‘ARAFAH

1.      Kufika mapema katika sehemu viliko viwanja vya ‘Arafah lakini wakawa nje ya Viwanja vya ‘Arafah hadi jua likazama. Kisha wakaondoka kwenda Muzdalifah hali ya kuwa hawajasimama katika Viwanja vya ‘Arafah. Na hili ni kosa kubwa ambalo linapotokea mtu anakuwa ameikosa Hijja kwani kusimama katika viwanja vya ‘Arafah ndiyo nguzo kubwa ya Hijja ambayo Hijja ya mtu haiswihi hadi mtu awe amesimama katika viwanja vya ‘Arafah. Mtume (Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallama) amesema kuwa: “Hijja ni ‘Arafah, atakayekuja usiku wa baada ya Mahujaji kusimama ‘Arafah lakini kabla ya kuchomoza Alfajiri ya tarehe 10 atakuwa ameidiriki ‘Arafah na Hijja yake itakuwa sahihi”.

2.      Kuondoka kwao katika viwanja vya ‘Arafah kabla ya kuzama jua. Na hii kosa kubwa tena ni haramu kwa kuwa kufanya hivyo ni kukhalifu amri ya Mtume (Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallama) kwani yeye Mtume (Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallama) alikaa katika viwanja vya ‘Arafah hadi jua likazama na giza likaanza kuingia ndipo akaondoka kuelekea Muzdalifah. Ama kuondoka kabla ya jua kuzama hii ni katika vitendo vya kijahiliya alivyokataza Mtume (Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallama).

3.      Baadhi ya Mahujaji kuelekea Jabal ‘Arafah wakati wa kuomba du’aa hata kama kwa wao kufanya hivyo wanakipa Qiblah mgongo au kinakuwa upande wa kulia au wa kushoto. Na hili ni kinyume na mwendo wa Mtume (Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallama), kwani Sunnah wakati wa kuomba du’aa hapo ni kuelekea Qiblah na si Jabal ‘Arafah au kilima cha ‘Arafah.

 

KUTUPA MAWE NA MAKOSA YAKE

1.      Baadhi ya watu kuitakidi kuwa ni lazima wachukue vijiwe kutoka Muzdalifah tu. Kwa itikadi yao hiyo wakawa wanajikalifisha na kuzichosha nafsi zao kwa kufanya hivyo.

2.      Itikadi yao kuwa wanapopiga minara ile ya Jamarati wanakuwa wanampiga Shetani. Hivyo mara nyingine utawasikia wakisema kuwa tumempiga Shetani mkubwa au mdogo au tumempiga baba wa Mashetani wakimaanisha ule mnara mkubwa yaani Jamaratul ‘Aqabah na mfano wa hivi. Na mingi ya mifano ambayo haifai katika sehemu hii tukufu.

3.      Kutupa mawe makubwa, viatu na hata miti. Hili ni kosa kubwa na linalokhalifu mafundisho ya Mtume (Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallama) ya kauli na vitendo.

4.      Kuziendea sehemu za kupiga mawe kwa vurugu na papara bila hata kuwahurumia waja wengine wa Allaah, jambo ambalo husababisha maudhi kwa Waislamu wengine na hata mara nyingine kutukanana na kupigana au hata vifo. Hali hii hugeuza sehemu hizi tukufu na kuwa kama sehemu za vurugu, kutukanana na mapambano.

5.      Kuacha kwao kuomba baada ya kutupa mawe mnara wa kwanza na wa pili katika yale masiku yanayoitwa Ayyaamu Ttashriyq au masiku matatu ya kutanda nyama. Ilivyothibiti ni kuwa Mtume (Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallama) alikuwa pindi akimaliza kupiga mawe minara miwili ya kwanza alikuwa akisimama baada ya kupiga kila mmoja ya minara hii miwili ya mwanzo akielekea Qiblah na kunyanyua mikono yake na kuomba du’aa ndefu.

6.      Kutupa mawe yote kwa mkupuo mmoja. Na hili ni kosa kubwa sana. Wanachuoni wanasema kuwa ikiwa mtu atatupa mawe yote kwa mkupuo mmoja basi hiyo itahesabiwa kuwa ametupa jiwe moja.

7.      Kuzidisha kwao du’aa wakati wa kutupa mawe, yaani du’aa ambazo hazikuthibiti wakati wa Mtume (Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallama) kama kusema kwao; “Ee Mwenyezi Mungu yajaalie mawe hayo kuwa ni radhi kwako na ni ghadhabu kwa Shetani”. Mara nyingine wao huacha Takbira iliyothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallama). Na haya ni makosa kishari’ah.

8.      Watu wengine kutaka kutupiwa mawe hata kama hawana udhuru wa kishari’ah. Hii inaweza kuwa ni kwa sababu ya kukwepa zahma na misongamano. Na hili linakuwa ni kinyume na mafundisho ya Mtume (Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallama) na alivyoagiza.

BAADHI YA MATUKIA YA KUFANYA WAKATI WA HIJJA

Hajj

 
 
 

1 – 7 Dhul-Hijjah – Makkah au Madiynah

Kuzuru Msikiti wa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم au kuweko Makkah kufanya 'Umrah (kwa Wanaofanya Hajjut-Tamattu'u) na kuendelea kuswali hapo Masjidul-Haraam.

Madiynah

  Kuswali Masjidun-Nabawiy na wanaume kuzuru kaburi la Mtume صلى الله عليه وآله وسلم

Makkah

Kufanya Twawwaaf Kuzunguka Ka'abah mara 7 Kuswali Raka'ah mbili Maqaam Ibraahiym Sa'yi - Swafaa Na Marwah Kuanza Kilima cha Swafaa kwenda kilima cha Marwah mara saba. Wakimaliza 'Umrah watabakia Makkah na kuswali katika Masjidul-Haraam kupata fadhila zake

8 Dhul-Hijjah – Mina

Asubuhi Wanaondoka Makkah kuelekea Minaa. kwa makadirio ni 8km

9 Dhul-Hijjah –

Siku ya 'Arafah Wanaondoka kutoka Minaa asubuhi kuelekea 'Arafah na kubaki hadi jua litakapozama. Na umbali unakadiriwa 14km Ni siku ya kutekeleza fardhi kubwa miongoni mwa taratibu za Hajj. Siku ya kuomba Du'aa sana. Na ndiyo siku iliyokamilika Dini yetu tukufu aliposimama Mtume صلى الله عليه وآله وسلم katika mlima wa 'Arafah na kutoa khutbah yake ya mwisho. Na ni siku ambayo wengi wetu wataachiwa huru na moto. Hapa wataswali Swalah ya Adhuhuri na Alasiri 'jam'an wa Qaswran' (kujumuisha na kufupisha Rakaah mbili mbili). Watasikiliza khutbah (watakaojaaliwa kuweko karibu na Masjidun-Namirah). Wasiokuwepo huko siku hiyo watafunga Swawm ya 'Arafah ambayo Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kasema inafuta madhambi ya mwaka uliopita na ujao. Jua likizama, wataelekea Muzdalifah.

10 Dhul-Hijjah – Muzdalifah – Mina - Makkah

Watafika Muzdalifah usiku na wataswali Magharibi na 'Ishaa 'jam'an wa Qaswran' (kujumuisha na kufupisha Rakaah mbili mbili) Watabakia Muzdalifah usiku mzima kwa kumkumbuka Allaah سبحانه وتعالى sana na kuokota vijiwe vya kurusha katika Jamaraat. Asubuhi – Yawmun-Nahr (siku ya kuchinja) kwa Mahujaji, na kwa wasiokuwepo huko ni siku ya 'Iyd. Wataelekea kutekeleza vitendo vifuatavyo vya fardhi za Hajj:
1) Kurusha vijiwe katika Jamaraat
2) Kutufu Twaaful-Ifaadhwah
3) Kunyoa nywele
4) Kuchinja (vyovyote watakavyotanguliza katika vitendo hivi inajuzu) Kurusha mawe katika Jamaraat

11 – 12 Dhul-Hijjah – Ayyaamut-Tashriyq (Siku ya kwanza na ya pili ya Tashriyq)

Watarudi Minaa na kwa ajili ya kurusha mawe katika Jamaraat. Ni siku za kula na kunywa na kumkumbuka sana Allaah  سبحانه وتعالى

13. Dhul-Hijjah (Siku ya mwisho ya Tashriyq)

Wanaopenda kubakia Mina watabakia kisha watarudi Makkah na ikiwa safari imewadia watafanya Twawwaaful-Wida'a (Twawwaaf ya kuaga)