Monday, October 01, 2012

BAADHI YA MATUKIA YA KUFANYA WAKATI WA HIJJA

Hajj

 
 
 

1 – 7 Dhul-Hijjah – Makkah au Madiynah

Kuzuru Msikiti wa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم au kuweko Makkah kufanya 'Umrah (kwa Wanaofanya Hajjut-Tamattu'u) na kuendelea kuswali hapo Masjidul-Haraam.

Madiynah

  Kuswali Masjidun-Nabawiy na wanaume kuzuru kaburi la Mtume صلى الله عليه وآله وسلم

Makkah

Kufanya Twawwaaf Kuzunguka Ka'abah mara 7 Kuswali Raka'ah mbili Maqaam Ibraahiym Sa'yi - Swafaa Na Marwah Kuanza Kilima cha Swafaa kwenda kilima cha Marwah mara saba. Wakimaliza 'Umrah watabakia Makkah na kuswali katika Masjidul-Haraam kupata fadhila zake

8 Dhul-Hijjah – Mina

Asubuhi Wanaondoka Makkah kuelekea Minaa. kwa makadirio ni 8km

9 Dhul-Hijjah –

Siku ya 'Arafah Wanaondoka kutoka Minaa asubuhi kuelekea 'Arafah na kubaki hadi jua litakapozama. Na umbali unakadiriwa 14km Ni siku ya kutekeleza fardhi kubwa miongoni mwa taratibu za Hajj. Siku ya kuomba Du'aa sana. Na ndiyo siku iliyokamilika Dini yetu tukufu aliposimama Mtume صلى الله عليه وآله وسلم katika mlima wa 'Arafah na kutoa khutbah yake ya mwisho. Na ni siku ambayo wengi wetu wataachiwa huru na moto. Hapa wataswali Swalah ya Adhuhuri na Alasiri 'jam'an wa Qaswran' (kujumuisha na kufupisha Rakaah mbili mbili). Watasikiliza khutbah (watakaojaaliwa kuweko karibu na Masjidun-Namirah). Wasiokuwepo huko siku hiyo watafunga Swawm ya 'Arafah ambayo Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kasema inafuta madhambi ya mwaka uliopita na ujao. Jua likizama, wataelekea Muzdalifah.

10 Dhul-Hijjah – Muzdalifah – Mina - Makkah

Watafika Muzdalifah usiku na wataswali Magharibi na 'Ishaa 'jam'an wa Qaswran' (kujumuisha na kufupisha Rakaah mbili mbili) Watabakia Muzdalifah usiku mzima kwa kumkumbuka Allaah سبحانه وتعالى sana na kuokota vijiwe vya kurusha katika Jamaraat. Asubuhi – Yawmun-Nahr (siku ya kuchinja) kwa Mahujaji, na kwa wasiokuwepo huko ni siku ya 'Iyd. Wataelekea kutekeleza vitendo vifuatavyo vya fardhi za Hajj:
1) Kurusha vijiwe katika Jamaraat
2) Kutufu Twaaful-Ifaadhwah
3) Kunyoa nywele
4) Kuchinja (vyovyote watakavyotanguliza katika vitendo hivi inajuzu) Kurusha mawe katika Jamaraat

11 – 12 Dhul-Hijjah – Ayyaamut-Tashriyq (Siku ya kwanza na ya pili ya Tashriyq)

Watarudi Minaa na kwa ajili ya kurusha mawe katika Jamaraat. Ni siku za kula na kunywa na kumkumbuka sana Allaah  سبحانه وتعالى

13. Dhul-Hijjah (Siku ya mwisho ya Tashriyq)

Wanaopenda kubakia Mina watabakia kisha watarudi Makkah na ikiwa safari imewadia watafanya Twawwaaful-Wida'a (Twawwaaf ya kuaga)

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO