Saturday, December 15, 2012

MAKAO MAKUU YA IKHWANUL MUSLIMIN


Makao makuu ya Ikhwanul Muslimin yamechomwa moto tena huko Misri. Duru ya kuaminika kutoka Misri imeripoti kuwa watu wasiofahamika wamechoma moto  makao makuu ya harakati ya Ikhwanul Muslimin katika mkoa wa Kafr Sheikh huko Misri. Ripoti zinasema kuwa hadi sasa ofisi 28 zenye mfungamano na Ikhwanul Muslimin zimechomwa moto katika mikoa tofauti ya Misri na watu wasiopungua saba wameuliwa katika mapigano ya hivi karibuni nchini humo. 
Wakati huo huo Ikhwanul Muslimin imeituhumu Imarati kuwa imewauwa viongozi watatu wa kundi hilo. 

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO