Thursday, January 03, 2013

HAMAS YAJIANDAA KUIVAA TENA ISRAEL


Naibu Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesema mapambano ya intifadha ya 3 ya Palestina yako njiani. Musa Abu Marzuq ameongeza kuwa, ili kupatikana uhuru na kujikomboa, hivi sasa taifa la Palestina linahitajia silaha za muqawamah katika kukabiliana na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Wakati hayo yakiripotiwa Marekani imewataka viongozi wa Palestina na utawala wa Kizayuni wa Israel waupokee mwaka huu wa 2013 kwa kuanzisha tena mazungumzo ya moja kwa moja kati yao.
Mazungumzo eti ya amani kati ya Israel na Wapalestina yamegonga ukuta tangu Septemba mwaka 2010, sababu kubwa ikiwa ni kuendelea Tel Aviv na siasa zake za kupanua vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi ya Palestina.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO