Monday, January 21, 2013

OBAMA KULA KIAPO TENA


Rais Barack Obama wa Marekani anatazamiwa kula kiapo tena leo katika sherehe itakayohudhuriwa na umma mjini Washington. Obama aliapishwa kwa mara ya kwanza hapo jana kuanza muhula wa pili wa miaka minne kama rais wa Marekani, katika sherehe ndogo iliyohudhuriwa na mkewe, Michelle Obama pamoja na mabinti zao, Sasha na Malia.
Kulingana na katiba ya Marekani, marais hula kiapo tarehe 20 Januari baada ya kuchaguliwa kwake, lakini kwa vile tarehe hiyo ilikuwa Jumapili, sherehe rasmi zimesogezwa hadi leo Jumatatu. Watu zaidi ya milioni moja wanatarajiwa kushiriki sherehe hizo mjini Washington.
Miongoni mwa mambo yatakayopewa kipaumbele na Rais Obama katika muhula huu wa pili ni kushughulikia nakisi katika bajeti, na mapambano dhidi ya umilikaji holela wa bunduki, kufuatia mauaji mabaya kwenye shule ya msingi mwezi uliopita.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO