Sunday, February 10, 2013

ALSHABAB WASHAMBULIA JESHI LA ETHIOPIA

Wapiganaji wa Al Shabab wametekeleza shambulizi la kuvizia dhidi ya wanajeshi wa Ethiopia katike eneo la Bakool kusini magharibi mwa Somalia. Duru zinaarifu kuwa wapiganaji wa Al Shabab walitekeleza shambulizi hilo siku ya Alkhamisi wakati wanajeshi wa Ethiopia walipokuwa wakirejea katika kituo chao baada ya kupiga doria katika mji wa El Barde.

 Shambulizi hilo la kuvizia limejiri karibu na kijiji cha Yed kilicho baina ya mji wa El Barde na ule wa Hudur ambao ni makao ya wanajeshi hao wa Ethiopia. Walioshuhudia tukio hilo wanasema idadi isiyojulikana ya wanajeshi wa Ethiopia na wapiganaji wa Al Shabab wameuawa. Siku ya Jumatano pia gari la wanajeshi wa Ethiopia lilishambuliwa huko Baidoa mji mkuu wa eneo la Bay. Wanajeshi wawili wa Ethiopia waliuawa katika hujuma hiyo. Pamoja na kuwa wapiganaji wa Al Shabab walipokonywa udhibiti wa mji wa Baidoa na maeneo mengine ya Somalia, lakini bado wanatekeleza mashambulizi ya kuvizia dhidi ya vikosi vya kigeni nchini humo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO