Sunday, February 03, 2013

MRADI WA NYUKLIA WA IRAN KUGUBIKA MKUTANO WA USALAMA DUNIANI

Mkutano wa 49 kuhusu usalama duniani unamalizika hii leo mjini Munich.Mada kuu mnamo siku hii ya mwisho ya mkutano huo inahusu mradi wa kinuklea wa Iran.Hotuba zilizokuwa zikisubiriwa kwa hamu ni  pamoja na ile ya waziri wa mambo ya nchi za nje wa Iran Ali Akbar Salehi na ya waziri wa ulinzi wa Israel  Ehud Barack. Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Iran Ali  Akbar Salehi amewaambia wajumbe mkutanoni duru ijayo ya mazungumzo kuhusu mradi wake wa kinuklea itafanyika February 25 nchini Kazakhstan. Na waziri wa ulinzi wa Israel,Ehud Barak  amesema nchi yake pamoja na washirika wao wamedhamiria kuizuwia Iran isitengeneze bomu la kinuklea.Amesema Iran yenye nguvu za kinyuklea itamaanisha mwisho wa makubaliano ya kutosambaza silaha na sio tu katika eneo hilo bali kote ulimwenguni.Miezi iliyopita Israel imekuwa mara kwa mara ikitishia kufanya hujuma za kijeshi dhidi ya Iran kuizuwia nchi hiyo isitengeneze bomu la kinuklea.Katika mjadala kuhusu mzozo wa Syria hapo jana,wawakilishi hawajafanikiwa kusawazisha misimamo yao.Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Urusi Serguei Lavrow ameonya kwa mara nyengine tena dhidi ya kujiingiza katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.Pembezoni mwa mkutano huo,waziri  huyo wa mambo ya chi za nje wa Urusi alikutana kwa mara ya kwanza na viongozi wa upande wa upinzani wa Syria.Serguei Lavrow amesema atakua akikutana nao kila kwa mara siku za mbele.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO