Friday, February 08, 2013

MSHAURI WA OBAMA ASEMA MAREKANI INAKIUKA HAKI ZA BINADAMAU

Mshauri wa Rais Barack Obama wa Marekani kuhusu masuala ya ugaidi, John Brennan amesema mbinu zinazotumiwa na CIA kuwasaili washukiwa wa ugaidi ni kinyume cha sheria za kimataifa na mkataba wa Geneva. Brennan ameiambia kamati ya bunge kuhusu usalama kwamba katika kipindi cha utawala wa George Bush, washukiwa wa ugaidi waliteswa na haki zao kukiukwa wakati wa kusailiwa na maafisa wa CIA.
John Brennan ambaye amependekezwa kuchukua uongozi wa CIA amesema akipata nafasi hiyo atafanya juhudi kuona haki za binadamu na sheria za kimataifa zinaheshimiwa wakati wa kuwasaili washukiwa wa ugaidi.
Wakati wa utawala wa Busha, picha za aibu za jinsi maafisa wa Marekani walivyokuwa wakiwatesa washukiwa wa ugaidi ziliamsha hasira za walimwengu na kuzusha maandamano makubwa katika nchi mbalimbali duniani kulaani unyama huo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO