Saturday, March 02, 2013

JESHI HALINA NAFASI TENA SIASA YA MISRI


Msemaji wa harakati ya Ikhwanul Muslimin ya Misri amesema kuwa kipindi cha jeshi kujihusisha na masuala ya kisiasa nchini humo kimepita na wala hakitarejea. Ahmad Arif amesema kuwa taasisi ya jeshi la Misri inapaswa kuheshimu mipaka na kazi iliyoainishiwa na katiba ya nchi ambayo ni kulinda usalama wa Misri na kwamba kipindi cha jeshi kuingilia masuala ya kisiasa kimemalizika.
Msemaji wa harakati ya Ikhwanul Muslimin amelaani hatua ya baadhi ya makundi ya upinzani yaliyotoa wito wa kufanyika maandamano hii leo Ijumaa kwa ajili ya kulitaka jeshi liingilie tena masuala ya kisiasa nchini Misri na kusema wito huo ni juhudi zisizo na tija zinazokusudia kulitumbukiza jeshi katika malumbano ya kisiasa. Ahmad Arif amesema kuwa makundi yanayotoa wito huo yameshindwa katika masanduku ya kupigia kura na katika fikra za wananchi wengi wa Misri na kwa msingi huo yanataka kufanya mapinduzi dhidi ya maoni na maamuzi ya wananchi.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO