Wednesday, April 24, 2013

SAUDIA YASIMAMISHA UBOMOAJI WA MISIKITI YA KIZAMANI


Serikali ya Saudi Arabia imelazimika kuacha mpango wa kubomoa mahala alipozaliwa Mtume Mtukufu Muhammad SAW, ili kupanua ujenzi wa Masjidul Haraam baada ya hatua hiyo kukabiliwa na upinzani mkubwa wa wananchi na maulamaa wa nchi hiyo.
A'ref Qadhi Msaidizi wa Mkuu wa Baraza la Mji wa Makka anayehusika na masuala ya ustawi amesema kuwa, maktaba ya Makka haitabomolewa  kwani iko mahala  alipozaliwa Mtume SAW. Hii ni katika hali ambayo, Sheikh Abdul Aziz Aal Sheikh, Mufti wa Kiwahabi nchini Saudi Arabia alitoa fatuwa ya kuruhusu kubomolewa athari za Kiislamu kwa minajili ya kupanuliwa Masjidul Haram.
Naye Sheikh Abdul Wahhab Abu Suleiman ambaye ni miongoni mwa Maulamaa wa Baraza la Wanazuoni wa Kiislamu nchini humo amesema kuwa, kubomolewa maktaba hiyo ni sawa na kuondosha athari kubwa zaidi za kihistoria katika dini ya Kiislamu na kwamba suala hilo litaziumiza nyoyo za Waislamu ulimwenguni kote.
Licha ya kufeli zoezi hilo la kubomoa mahala alipozaliwa Mtume SAW, lakini athari nyingine nyingi za kale za Kiislamu zilizoko pambizoni mwa Masjidul Haram zimeshaharibiwa na kubomolewa kwa amri ya utawala kifalme wa Aal Saud.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO