Tuesday, May 14, 2013

ARAB LEAGUE YAKIRI KUSHINDWA KUIKABILI ISRAEL


Nabil al Arabi Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu amekiri kushindwa jumuia hiyo kuulinda mji wa Qud's unakaliwa kwa mabavu na Israel. Al Arabi amesema, jumuiya hiyo haina uwezo, suhula wala vifaa vya kuweza kuzuia jinai zinazotekelezwa na utawala wa Kizayuni wa Israel. Amesema hayo katika mkutano wa jumuiya hiyo mjini Cairo, ambako pia ametaka kuanza kuchukuliwa hatua za kisiasa na kidiplomasia za kuulazimisha utawala wa Kizayuni kusimamisha hujuma zake dhidi ya Wapalestina.
Baraza Kuu la Jumuiya ya Arab League lilihitimisha kikao chake hicho cha masaa mawili cha kujadili jinai za kila siku za Israel katika mji wa Quds Tukufu bila kutoa tamko lolote rasmi juu ya suala hilo.
Hayo yanajiri huku utawala wa Kizayuni wa Israel ukizidisha jinai za kila aina dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina wasio na ulinzi wowote.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO