Thursday, May 23, 2013

KESI YA UAMSHO KUHAMISHIWA DAR


Kesi ya uchochezi inayomkabili Kiongozi wa Jumuiya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu ya Zanzibar (Jumiki),Sheikh Faridi Hadi Ahmed (41), na wenzake 9, sasa imepangwa kuunguruma katika Mahakama ya Rufani Dar es Salaam, Juni 10, mwaka huu. Sheikh Faridi na wenzake wanakabiliwa na kesi hiyo katika Mahakama Kuu ya Zanzibar. Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mselem Ali Mselem, Mussa Juma, Azzan Khalid Hamdani, Suleiman Juma, Khamis Ali na Hassan Bakari, Ghalib Hamada Juma, Abdallah Saidi na Fikirini Fikirini.
Washtakiwa hao kupitia kwa mawakili wao, wamewasilisha maombi katika Mahakama ya Rufani Tanzania, wakiomba mahakama hiyo itupilie mbali rufaa ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Zanzibar, dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, wa Machi 11, mwaka huu. Mahakama hiyo, katika uamuzi wake uliotolewa na Jaji Abrahamu Mwampashi, ilitengua mwenendo wa maombi ya dhamana ya washtakiwa yaliyotolewa na na mawakili wao kwa Msajili wa Mahakama Kuu, Oktoba 25, siku washtakiwa hao waliposomewa mashtaka.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO