Saturday, May 18, 2013

KOREA KASKAZINI YAFYATUA MAKOMBORA YAKE

Korea Kaskazini leo imefyatua makombora matatu ya masafa mafupi ndani ya Bahari ya Japan, kama sehemu ya mazoezi ya kijeshi. Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Korea Kusini amesema makombora mawili yalifyatuliwa mapema leo na jingine moja likafyatuliwa saa za mchana. Amesema Korea Kusini inaendelea kuwa katika hali ya tahadhari ili kupambana na hali yoyote ya kitisho inayoweza kusababishwa na serikali ya Korea Kaskazini. Majaribio hayo yanafuatia mazoezi ya pamoja yaliyofanywa na jeshi la wanamaji la Marekani na Korea Kusini mapema wiki hii, na kushutumiwa na Korea Kaskazini kuwa ni uchokozi na matayarisho ya vita.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO