Sunday, May 19, 2013

MTUHUMIWA WA UGAIDI NA MKEWE WAUAWA NAIROBI


Mtuhumiwa mmoja wa ugaidi na mkewe wameuawa leo asubuhi mjini Nairobi Kenya. Vyombo vya habari nchini Kenya vimeripoti kuwa, mtuhumiwa huyo amepatikana na maguruneti katika eneo la Githurai Kimbo, mjini Nairobi. Taarifa zimeongeza kuwa, maafisa sita wa polisi wamejeruhiwa katika operesheni hiyo iliyodumu kwa karibu masaa manane.
Jeshi la Polisi la Kenya limesema kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa anapanga kufanya shambulio la kigaidi mjini Nairobi. Taarifa ya polisi imeongeza kuwa, mtuhumiwa huyo alianza kuwarushia maguruneti maafisa wa polisi na kuwajeruhi 6 kati yao ambao wamelazwa hospitalini. Mwili wa mtuhumiwa huyo na wa mkewe imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali moja mjini Nairobi. Inadaiwa kuwa mtuhumiwa huyo ana uhusiano na Elgiva Oliacha Bwite aliyetiwa mbaroni mjini Nairobi kwa tuhuma za kuhusiana na shambulio la kigaidi jijini Nairobi mwaka 2011.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO