Friday, May 24, 2013

WAAI WAUA WANAJESHI 18 NIGER


Wanajeshi 18 wa jeshi la Niger wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa, baada ya kundi linalobeba silaha lenye misimamo mikali nchini humo kushambulia kambi ya kijeshi iliyoko kaskazini mwa nchi hiyo. Taarifa zinasema kuwa, kambi hiyo ya kijeshi iko kwenye eneo linalochimbwa madini ya urani na shirika moja la Kifaransa.
Duru za kijeshi zinasema kuwa, mapigano makali yalijiri kati ya majeshi ya serikali na waasi hao, mara baada ya kutokea mlipuko wa bomu la kutegwa garini karibu na kambi hiyo ya kijeshi ya Agadez na kusababisha maafa makubwa kwa jeshi la nchi hiyo.
Duru hizo zimesema kuwa, wanajeshi 18 wa serikali na wanamgambo wanne wa kundi la waasi wenye misimamo mikali wameuawa kwenye mapigano hayo. Imeelezwa kuwa, mwanamgambo mmoja wa waasi anawashikilia mateka wanajeshi watatu kwenye nyumba moja iliyoko karibu na kambi hiyo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO