Wednesday, December 12, 2012

QURAN YAONGOZA KWA KUUZWA HISPANIA


Utafiti uliofanywa na taasisi ya Ant ya Uhispania umebaini kuwa Qur'ani Tukufu ndio kitabu kinachouzwa kwa wingi zaidi nchini humo katika nusu ya pili ya mwaka huu wa 2012.
Uchunguzi huo unaonesha kuwa vitabu vinavyohusu dini ya Uislamu ndivyo vilivyouzwa kwa wingi zaidi nchini Uhispania katika nusu ya pili ya mwaka huu.

Uchunguzi wa kituo hicho unasema kuwa, nakala za kitabu kitakatifu cha Qur'ani zinanunuliwa kwa wingi katika maduka ya vitabu ya Uhispania na kuwa kitabu kinachouzwa kwa wingi zaidi. Baada ya Qur'ani Tukufu kitabu cha Sira ya Ibn Hisham kinachozungumzia sira na historia ya Mtume na Uislamu kinafuatia kwa kuuzwa kwa wingi zaidi nchini Uhispania.
Uchunguzi huo pia umesema kuwa baada ya kuonyeshwa filamu inayomvunjia heshima Mtume Muhammad (saw) nchini Marekani uuzaji wa vitabu vinavyohusu dini ya Uislamu uliongezeka sana mwezi uliopita huko Uhispania ikilinganishwa na miezi mingine.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO