IRAN KUTUMA CHAKULA CHA MSAADA MYANMAR
Jumuiya ya Hilali Nyekundu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema itatuma shehena kubwa ya misaada ya kibinaadamu kwa ajili ya Waislamu wanaodhulumiwa nchini Myanmar.
Mkuu wa masuala ya habari katika Hilali Nyekundu ya Iran Pouya Hajian amesema shehena hiyo ya kwanza ya misaada inajumuisha tani 15 za vyakula na tani 15 za bidhaa nyingine za dharura.
Waislamu wa kabila la Rohingya nchini Myanmar wamekuwa wakikandamziwa na kuteswa katika nchi hiyo ya kusini mashariki mwa Asia inayotawaliwa na Mabuddha. Katika miezi ya hivi karibuni Mabuddha wenye misimamo mikali wamekuwa wakiwashambulia Waislamu na kuteketeza moto misikiti na nyumba zao.
Maelfu ya Waislamu wameuawa na makumi ya maelfu ya wengine kuachwa bila makao katika hujuma zinazotekelezwa na Mabudhha. Umoja wa Mataifa unasema Waislamu wa kabila la Rohingya nchini Myanmar ndio jamii inayokandamizwa zaidi duniani.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO