Sunday, December 09, 2012

NIJAAD: MATATIZO YA ULIMWENGUNI NI KUPENDA UKUBWA


Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa mivutano inayoendelea sasa  duniani inasababishwa na hatua ya baadhi ya nchi kupenda makuu.
Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa matatizo yanayoikabili dunia hii leo yanasababishwa na siasa za kupenda makubwa za baadhi ya nchi zinazotaka kuhodhi baadhi ya nchi nyinginezo ambazo lengo lake ni kupora maslahi ya mataifa mengine kwa kutoa nara na kaulimbiu za kutetea haki za binadamu na demokrasia.
Rais Ahmadinejad ameyasema hayo leo katika mazungumzo kati yake na  Liur Gurgan, Balozi Mpya wa Ireland hapa mjini Tehran. Rais wa Iran amesema ufumbuzi wa matatizo yanayoukabili ulimwengu hivi sasa  unahitajia kufanyiwa marekebisho muhimu katika mifumo ya kimataifa kwa mujibu wa uadilifu na kuongeza kuwa nchi za ulimwengu zinapasa kushirikiana bega kwa bega na kutotoa mwanya kwa  maisitikbari kuzitwisha nchi  hizo matakwa yao.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO