Mafuriko
makubwa huko Indonesia yaliyosababishwa na mvua kali za siku kadhaa yameuwa
watu wasiopungua 15 nchini humo. Watu wawili waliopoteza maisha yao huko
Jakarta na wengine wanne wa familia moja huko Semaranga makamao makuu ya mkoa
wa Java ni kati ya jumla ya watu 15 waliopoteza maishah yao kufuatia mafuriko
hayo yaliyoikumba Indonesia hivi karibuni. Johan Freddy Afisa wa Idara ya Taifa
ya Kushughulia Maafa ya Kitaifa ameeleza kuwa ramani yao inaonyesha kuwa
karibu asilimia 50 ya mji wa Jakarta uko chini ya maji. Ameongeza kuwa nyumba
zisizopungua laki moja zimejaa maji na hivyo kusababisha watu elfu kumi kuwekwa
katika makazi ya muda.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO