Viongozi
wa shule moja ya msingi mjini New York nchini Marekani wamethibitisha kutiwa
mbaroni mwanafunzi mmoja mwenye umri wa miaka saba akiwa ameficha bastola
iliyojaa risasi. Gazeti la Huffington Post linalochapishwa Marekani limeandika
kuwa, tukio hilo limetokea katika shule ya msingi ya Viaio iliyoko katika eneo
la Far Rockaway mjini New York. Mara baada ya kujiri tukio hilo, uongozi wa
shule hiyo ulichukua uamuzi wa kuifunga shule hiyo. Hata hivyo, uongozi wa
shule ulikataa kutaja jina la mwanafunzi huyo na jinsi walivyoigundua silaha
hiyo. Tukio hilo linatokana na maombi ya mara kwa mara yanayotolewa na wazazi
na wananchi kutaka zichukuliwe hatua kali za kudhibiti uingizwaji silaha
mashuleni unaofanywa na wanafunzi au wahalifu kama ilivyotokea hivi karibuni
kwenye shule ya msingi ya Sindy Hook, ambapo wanafunzi 20 na wafanyakazi
6 waliuawa. Tukio la kukamatwa silaha kwa mwanafunzi mwenye umri wa miaka saba,
linaonyesha kuwa, viongozi wa Marekani bado hawajawa jaddi katika kuzuia
ubebaji silaha mashuleni, kinyume na madai yanayotolewa na Rais Barack Obama wa
nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO