Tuesday, January 01, 2013

ATHENS MJI PEKEE USIO NA MSIKITI

Waislamu katika mji mkuu wa Ugiriki Athens wameendelea kunyimwa haki zao za kimsingi likiwemo suala la kuwa na maeneo yao ya kufanyia ibada na shughuli za kidini. Makundi yenye kufurutru ada ambayo yanapinga Uislamu yamezuia kabisa Waislamu kupatiwa haki zao za kimsingi na hivyo kuufanya mji wa Athens kuwa ndio mji mkuu pekee barani Ulaya ambao hauna msikiti. Ripoti zinaonesha kuwa, tangu jamhuri ya kwanza ya Ugiriki ipatikane  mwaka 1832 hadi sasa, hakuna serikali au utawala ambao umeruhusu kujengwa Msikiti mjini Athens. Waislamu wa Athens ambao wanapindukia laki tatu wameendelea kuilalamikia serikali ya nchi hiyo kutokana na kutoandaa mazingira ya kupatikana eneo la ibada kwa ajili yao.  Viongozi wa kanisa wanadai kwamba, kuruhusiwa Waislamu kujenga Misikiti ni sawa na kuchukua hatua za kubadilisha utambulisho wa Kikristo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO