Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itafungua kambi maalumu nchini Myanmar
kwa lengo la kuwasaidia Waislamu wanaodhulumiwa nchini humo. Hayo yamedokezwa
na Mansour Haqiatpour, Naibu Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama wa Taifa na Sera
za Kigeni katika Bunge la Iran. Amesema kufuatia mazungumzo na wakuu wa
Myanmar, Iran imeruhusiwa kuanzisha kambo katika jimbo la Rakhine ili
kuwahudumia maelfu ya Waislamu wa kabila la Rohingya. Mapema mwezi huu wabunge
kadhaa wa Iran walitembelea Myanmar kuchunguza hali ya Waislamu nchini humo na
kutathmini njia za kuwasaidia. Karibu Waislamu 800,000 wa kabila la Rohingya
nchini Myanmar wamekuwa wakikandamizwa na Mabudhaa wenye misimamo ya kufurutu
mipaka. Mabudhaa hao wameteketeza moto vijiji na misikiti ya Waislamu. Aidha
serikali ya Myanmar inatuhumiwa kuwa imekataa makusudi kuwasaidia Waislamu hao
walio wachache nchini humo. Maelfu ya Waislamu wa kabila la Rohingya wameuawa
na makumi ya maelfu ya wengine kuachwa bila makao katika miezi ya hivi
karibuni.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO