Wednesday, January 16, 2013

IRAN KUTUPILIA MBALI MATUMIZI YA EURO NA DOLLAR


Waziri wa Masuala ya Uchumi na Fedha Iran Shamsuddin Husseini amesema kuwa, Iran ina mpango wa kuacha kutumia sarafu za euro na dollar katika biashara ya kimataifa.
Amesema uamuzi huo umechukuliwa kufuatia hatua ya Marekani na Umoja wa Ulaya kuiwekea Iran vikwazo. Shamsuddin Husseini amesema kuwa, hatua ya Iran ya kubadilisha mfumo wa kibiashara itapelekea nchi hii kutohitajia sarafu za euro na dollar katika biashara.
Amesema kuwa, washirika wa kibiashara wa Iran wamekaribisha uamuzi huo wa kutupilia mbali sarafu hizo mbili za kigeni. Amesema mgogoro wa kifedha barani Ulaya na Marekani ni jambo ambalo limepelekea nchi nyingi kuunga mkono hatua ya Iran ya kutupilia mbali sarafu za euro na dollar.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO