Saturday, January 12, 2013

MAREKANI ITAKUWA MSAIDIZI TU AFGHANISTAN

Kwa mujibu wa Rais Barack Obama ,vikosi vya Marekani vitaanza mapema,kuliko ilivyopangwa,kuwajibika kama "wasaidizi" tu nchini Afghanistan.Miezi mitatu kutoka sasa,wanajeshi wa Marekani watakuwa wakisimamia majukumu mengine kabisa ya yale waliyokuwa nayo hadi sasa" amesema Rais Obama baada ya mazungumzo yake pamoja na Rais Hamid Karzai wa Afghanistan mjini Washington.Jukumu la wanajeshi wa Marekani litakuwa kuwapatia mafunzo na ushauri wanajeshi wa Afghanistan.Wanajeshi wa Afghanistan walipangiwa hapo awali kuanza kudhamini wenyewe usalama wa nchi yao,kuanzia msimu wa kiangazi mwaka huu.Kwa jumla Rais Barack Obama amesifu mchango wa vikosi vya kimataifa nchini Afghanistan.Anasema wakaazi wengi  wa Afghanistan wanaiangalia nchi yao hii leo kuwa ni mahala salama pa kuishi.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO