Saturday, January 19, 2013

MAREKANI NAO KUINGIA MALI

Afisa mmoja wa kijeshi nchini Marekani amesema kuwa, Washington itaisadia Ufaransa katika vita vyake nchini Mali. Afisa huyo ameongeza kuwa, Marekani itaipatia Paris ndege za kusafirishia vifaa na wanajeshi kwa ajili ya kuendeshea shughuli za kukabiliana na waasi huko nchini Mali. Aidha amesema kuwa, tayari serikali ya Washington imekwisha kubaliana na viongozi wa Ufaransa kuhusiana na suala hilo na kwamba, kinachojiri hivi sasa kati ya viongozi wa pande mbili ni kujadili baadhi ya vipengee vya msaada huo. Jana Waziri wa Ulinzi wa Marekani Leon Panetta alitangaza kuwa, suala la Marekani kuipatia Ufaransa msaada wa kijeshi bado linajadiliwa. Hata hivyo baadhi ya wabunge wa Marekani wanapinga suala la kuendeshwa oparesheni za nchi kavu huko Mali. Oparesheni za Ufaransa dhidi ya waasi wanaoyadhibiti maeneo ya kaskazini mwa Mali, zimepelekea kushadidi hali ngumu ya maisha kwa raia wa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO