Wednesday, January 16, 2013

MALALAMIKO YA WAMAREKANI JUU YA UUZWAJI SILAHA

Makumi ya wakazi wa mji wa Newton nchini Marekani wameandamana kupinga uuzaji silaha kwenye maduka makuu nchini humo.  Wakazi wa mji wa Newtown jana waliandamana hadi mbele ya maduka makuu ya Walmart na kulaani uuzaji wa silaha katika maduka hayo. Waandamanaji hao walipiga nara wakitaka kusimamishwa uuzaji wa silaha kwenye maduka makuu ya Walmart. Itakumbukwa kuwa jumla ya watu 26 wakiwemo watoto 14 waliuliwa kwa kupigwa risasi mwezi Disemba mwaka jana na kijana aliyekuwa na umri wa miaka 20. Weledi wa mambo wanaamini kuwa sababu ya kuongezeka vitendo vya utumiaji mabavu huko Marekani ni kujiweka mbali raia wengi wa nchi hiyo na thamani za kiutu na kuenea kwa tabia ya kupenda vitendo vya kikatili na utumiaji nguvu tangu umri wa udogoni. 
  Kwa upande wapili  pia Jimbo la New York nchini Marekani limepitisha sheria mpya ya kudhibiti umiliki wa bunduki. Sheria hiyo imepitishwa ikiwa ni mwezi mmoja baada ya mtu mmoja aliyekuwa na bunduki kuwaua kwa kuwapiga risasi watoto 20 na walimu sita wa shule ya msingi katika eneo la Connecticut. Sheria hiyo inajumuisha kupiga marufuku kabisa kuuza bunduki za aina ya kijeshi na inaweka kiwango cha risasi hadi saba tu badala ya kumi. Wataalamu wa magonjwa ya akili sasa wanapaswa kutoa taarifa za wagonjwa kwa maofisa iwapo wanaaminika kuleta madhara kwao wenyewe au kwa watu wengine. Baadaye leo, Rais Barack Obama anatarajiwa kutoa tamko kuhusiana na hatua za kuchukua kupambana na ghasia zinazosababishwa na matumizi ya bunduki nchini Marekani.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO