Saturday, January 12, 2013

WANAWAKE KUSHIRIKI KWENY BARAZA LA USHAURI

Mfalme Abdullah bin Abdulaziz wa Saudi Arabia  ametoa amri ya kuingizwa wanawake kwenye Baraza la Ushauri la nchi hiyo ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya Saudi Arabia, kwa wanawake kuingizwa kwenye chombo hicho. Mfalme Abdullah alikifanyia marekebisho kipengee cha katiba kinachohusiana na  Baraza la Ushauri la nchi hiyo na kuandaa mazingira ya kuingizwa asilimia ishirini ya wanawake kwenye baraza hilo. Hali kadhalika Mfalme wa Saudi Arabia amewateua wajumbe 150 wa Baraza jipya la Ushauri wakiwemo wanawake. Wajumbe wa Baraza la Ushauri la Saudi Arabia huteuliwa na mfalme na wala hawachaguliwi na wananchi kama ilivyozoeleka katika nchi nyingi duniani. Inafaa kuashiria hapa kuwa, tarehe 25 Septemba 2011, Mfalme wa Saudi Arabia alitoa ruhusa kwa wanawake kushiriki kwenye chaguzi za mabaraza ya miji na vijiji. Amri ya Mfalme wa Saudia ya kushirikishwa wanawake kwenye baraza la ushauri imetolewa katika hali ambayo, wanawake nchini humo wanapigwa marufuku kujishughulisha na shughuli za kijamii, likiwemo hata suala la kuendesha magari.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO