Thursday, February 07, 2013

WASYRIA WAVAMIA MITANDAO YA ISRAEL

Katika toleo lake la jana gazeti la Maariv la Wazayuni limefichua kuwa, wavamizi wa mitandao kutoka Syria, wameweza kudukua (hack) maelfu ya mitandao mbalimbali ikiwemo ya kibiashara ya Israel, kama nji moja wapo ya kujibu mashambulizi ya hivi karibuni ya ndege za Wazayuni dhidi ya Syria. Gazeti hilo limefafanua zaidi kuwa, kwa mujibu wa vyanzo vya kiutaalamu vya utawala huo, wadukuzi hao wa Syria, wameweza kufunga mitandao ya Israel huku wakiacha ujumbe ulioeleza kuwa, Israel ni mbeba dhima ya mashambulizi ya ndege zake dhidi ya kiwanda cha utafiti huko karibu na mji mkuu wa Syria. Aidha wadukuzi hao wameeleza kuwa, wataendelea na hatua hiyo kuilenga mitandao ya mawasiliano ya utawala haramu wa Kizayuni. Gazeti hilo limemnukuu mkuu wa shirika la Midsack linalohusika na mawasiliano katika utawala huo akisema kuwa, hii ni mara ya kwanza kwa wadukuzi wa Syria kushambulia mitandao ya Israel na kuongeza kuwa, miongoni mwa mitandao muhimu iliyoshambuliwa na wadukuzi hao ni pamoja na kituo cha Kompyuta cha Israel na mitandao ya kitalii. Amesisitiza kuwa, wadukuzi pia wameweza kupata anuani mbalimbali, zikiwemo anuani nyengine za mitandao ya elektroniki sambamba kabisa na kupata taarifa za watu muhimu wa Israel. 

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO