Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani, John Kerry, amemtaka Rais Bashar al-Assad wa Syria ajiuzulu. Kerry aliyekuwa akizungumza baada ya kukutana na Waziri mwenzake wa Jordan, Nasser Judeh, alisema Assad anapaswa kuondoa matumaini ya kushinda vita hivyo na badala yake akubali kuondoka madarakani. Akaongeza kwamba anaamini kutokana na hali ya mambo nchini Syria kiongozi huyo hawezi kujinusuru.
Waziri huyo wa mambo ya nchi za nje wa Marekani akadokeza kwamba nchi yake na Jordan zinaweza kuchukua hatua mpya kuishawishi Urusi, mshirika mkubwa wa Syria, kumshinikiza zaidi Rais Assad aondoke madarakani. Kerry alisema Mfalme Abdullah wa pili wa Jordan anatarajia kuitembelea Urusi. Wakati huo huo, waasi kaskazini mwa Syria wameiteka kambi moja ya kijeshi, ikiwa ni hatua ya mafanikio ya tatu makubwa katika uwanja wa mapambano kwa siku kadhaa.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO