Tuesday, February 12, 2013

MAREKANI KUPUNGUZA VIKWAZO KWA SUDAN


Mwandiplomasia wa ngazi ya juu wa Marekani nchini Sudan amesema kuwa, karibuni hivi Washington itabadilisha sheria za vikwazo ambazo zitaziruhusu taasisi za kielimu katika nchi mbili za Sudan kushirikiana. Katika kile kinachoonekana wazi kuwa ni kujipa haki ya kuingilia masuala ya nchi nyingine, mwaka 2010  Marekani ilitangaza kuwa inapunguaza vikwazo katika masuala ya zana za kilimo na huduma nyingine na kuruhusu makampuni 6 kupata leseni za usafirishaji nje bidhaa zao. Mwanadiplomasia wa Marekani nchini Sudan Joseph D. Stafford amedai kuwa, serikali ya Obama inajiandaa kufanya mazungumzo mapana na ya wazi na Khartoum ili kujadili masuala yote yanaokwamisha kuhuishwa uhusiano kati ya nchi mbili hizo. Stafford amedai kuwa ushirikiano wa kiusalama kati ya pande mbili ambao umeimarika kwa zaidi ya muongo mmoja uliopita unaendelea na amedai ni wa kuridhisha.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO