Thursday, February 07, 2013

NAM YALAANI UCHOKOZI WA ISRAEL

Harakati ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote NAM imelaani hatua ya utawala wa Kizayuni ya kukiuka anga ya Syria na kukishambulia kituo cha utafiti wa kisayansi huko katika viunga vya Damascus. Watu saba waliuawa na kujeruhiwa katika mashambulizi hayo ya utawala wa Kizayuni. Harakati ya NAM imeitaja hatua hiyo kuwa ni uvunjaji wa wazi wa sheria za kimataifa na ukiukaji wa misingi na malengo ya hati ya Umoja wa Mataifa. Jumuiya ya NAM imesema iko pamoja na Syria na kusisitiza kuwa kuna udharura wa kuwajibika utawala wa Kizayuni kwa hatua zake hizo za kichokozi na athari zake. Jumuiya ya NAM pia imelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kulaani wazi wazi chokochoko hizo za Israel na kutekeleza wadhifa wake bila upendeleo. 

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO