Mkimbiaji Wesley Kipchumba Korir wa Kenya bingwa wa mbio za Boston Marathon za mwaka 2012 wiki hii andika historia mpya katika uwanja wa siasa baada ya kunyakua ushindi wa kiti cha ubunge wa Cherengany katika uchaguzi mkuu nchini Kenya uliofanyika siku ya Jumatatu iliyopita. Korir 28 ambaye alitumbukia kwenye kinyang'anyiro hicho akiwa mgombea binafsi alisema kuwa, alikuwa anapenda sana kuwa mwanasiasa tokea akiwa mdogo, lakini alikuwa akisubiri fursa ili aweze kujitumbukiza rasmi kwenye ulingo huo. Wesley Korir ambaye aliishi Marekani kwa ajili ya masomo ya elimu ya juu, mwaka jana aliibuka mshindi wa medali ya dhahabu katika mashindano ya mbio za Boston Marathon baada ya kutumia muda wa masaa 2: dk 12 sekunde 40. Mkimbiaji huyo amesema kuwa, licha ya kuwahudumia wananchi wa eneo lake bungeni, ataendelea pia kushiriki kwenye michuano mbalimbali ya mbio za Marathon. Wesley Korir amethibitisha kwamba atashiriki kwenye michuno ya mbio za Boston Marathon zitakazofanyika mwezi Aprili mwaka huu.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO