Jeshi la Nchi Kavu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limeanza mazoezi ya siku tatu katika mkoa wa Khuzestan, kaskazini mashariki mwa nchi. Kamanda wa kikosi cha nchi kavu katika Jeshi la Iran Brigedia Jenerali Ahmadreza Pourdastan amesema mazoezi hayo yaliyopewa jina la Khatam al-Anbia yameanza siku ya Jumamosi.
Kamanda huyo amesema luteka hiyo itajumuisha mazoezi ya vifaru, mizinga n.k. Naye Naibu Kamanda wa kikosi cha nchi kavu katika Jeshi la Iran Brigedia Jenerali Kioumars Heidari amesema makombora mapya yatafanyiwa majaribio katika mazoezi hayo. Amesema makombora hayo tayari yameshafanyiwa majaribio katika maabara na sasa yatafanyiwa majaribio katika eneo wazi. Katika miaka ya hivi karibuni Iran imekuwa ikifanya mazoezi ya kijeshi baharini, angani na nchi kazi. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mwa kwa mara imesisitiza kuwa uwezo wake mkubwa wa kijeshi ni wa kujihami.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO