Kiongozi wa Taifa la Korea Kaskazini Kim Jong-Un ameagiza roketi za nchi hizo ziwe tayari kwa mashambulizi kulenga kambi za kijeshi za Marekani pamoja na kuwashambulia washirika wao Korea Kusini. Tamko hilo limezidisha hofu ya usalama wa dunia kutokana na wengi kuhisi huenda mataifa hayo mawili ambayo yanamiliki silaha za maangamizi wakazitumia wakati wa vita na kuelta madhara si tu kwa wananchi lakini kwa mazingira.
Kim ametoa agizo hilo kutokana na kukerwa na kitendo cha majeshi ya marekani na yale ya Korea Kusini kuendelea na mazoezi yao ambayo Korea Kaskazini imeyaita yakichokozi na yanalengo la kutaka kuishambulia nchi yao. Agizo hilo limekuja kipindi hiki ambacho Waziri wa Ulinzi wa Marekani Chuck Hagel akiwa ziarani katika eneo la Peninsula na kusema Washington haiwezi ikawa muonga kutokana na vitisho vya Pyongyang. Mapema serikali ya Korea Kaskazini ilishatishia kufanya mashambulizi kulenga kambi za kijeshi za Marekani huko Japan kutokana na kukerwa na tabia ya nchi hiyo kuendelea kuifuatia kwenye shughuli zao za majaribio ya makombora ya nyuklia. Kwa upande wake Korea Kusini yenyewe imeendelea kusisitiza kuwa haiogopi vitisho hivyo na badala yake wametoa wito kwa Serikali ya Kim, kuachana na mpango wake wa Nyuklia ili kurudi karibu na jumuiya ya kimataifa. Juma hili pia Korea Kaskazini ilitangaza kukata njia zote za mawasiliano ya kijeshi na majirani zao ikiwa ni hatua za awali katika kutekeleza kile ambacho imeahidi kukitekeleza katika siku chache zijazo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO