Viongozi wa nchi 33 akiwemo Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran wanahudhuria mazishi ya hayati rais wa Venezuela Hugo Chavez ambayo yanafanyika leo Ijumaa. Ripoti zinasema tayari watu milioni mbili wameshauona mwili wa Chavez ambao umelazwa katika kituo cha kijeshi mjini Caracas.
Makamu wa Rais wa Venezuela Nicolas Maduro ambaye anashikilia nafasi ya urasi kwa muda ametangaza wiki mbili za maombolezo ya kitaifa kufuatia kifo cha Chavez ambaye aliaga dunia baada ya kuugua ugonjwa wa saratani kwa muda wa miaka miwili. Maafisa wa serikali ya Venezuela akiwemo makamu wa rais ameituhumu serikali ya Marekani kwa kumpa sumu Chavez na hivyo kusababisha kifo chake.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO