Harakati ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote NAM imetaka nchi zinazomiliki silaha za nyuklia kuziangamiza. Katika kikao cha dharura kilichofanyika Alkhamisi mjini New York NAM pia imetaka nchi ambazo zimetia saini Mkataba wa Kuzuia Usambazwaji Silaha za Nyuklia NPT zisaidiwe katika kutumia nishati ya nyuklia kwa malengo ya amani.
Balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa Mohammad Khazaee amesema kikao hicho kimehudhuriwa na mabalozi wa nchi za NAM. Ameongeza kuwa kikao hicho kiliitishwa kutathmini suala la Kongamano la Kuangalia Upya Mkataba wa Kuzuia Kuenea Silaha za Maangamizi ya Umati. Ameongeza kuwa marekebisho katika mkataba wa NPT yanapaswa kuzingatia suala la kuzishurutisha nchi zenye siasa za nyuklia kuangamiza silaha hizo pasina ubaguzi au undumakuwili. Khazaee pia amekosoa waliozuia kufanyika kongamano la Mashariki ya Kati Isiyo na Silaha za Nyuklia. Kongamano hilo lilikuwa lifanyike mwaka 2012 lakini kutokana na upinzani wa Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel kikao hicho hakikufanyika. Israel ndie mmiliki pekee wa silaha hatari za nyuklia katika eneo la Mashariki ya Kati.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO