Sunday, March 03, 2013
NIJAAD ASEMA MAADUI WATASHINDWA KUIZIBA MDOMO
Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, njama za maadui za kuzuia sauti ya taifa la Iran isiwafikie watu wengine ulimwenguni zitashindwa. Rais Ahmadinejad amesema hayo leo katika hafla ya ufunguzi wa kanali mbili za televisheni za Tamashaa na Salamat na kusisitiza kwamba, njama zinazofanywa na madola ya kibeberu za kuzuia risala ya Mwenyezi Mungu na ya kibinaadamu inayotangazwa na taifa la Iran isiwafikie walimwengu zitashindwa na kugonga mwamba. Rais Ahmadinejad ameashiria utendaji wa kindumakuwili wa madola ya Magharibi na hatua yao ya kukata matangazo ya kanali za televisheni na radio za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika satalaiti na kubainisha kwamba, muamala kama huo hauwezi kuzuia kuenea ujumbe wa Mwenyezi Mungu na wa kibinaadamu unaoenezwa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Rais wa Iran amesema kuwa, undumakuwili wa madola ya Magharibi katika kuvibinya na kuvibana vyombo vya habari vya Iran ni ithibati nyingine kwamba, madai ya madola hayo ya kupigia debe demokrasia ni porojo na urongo mtupu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO