Rais Barack Obama wa Marekani amewaonya wanaolivalia njuga kupindukia suala la nishati ya nyuklia ya Iran na kusisitizia umuhimu wa kutumika njia za kidiplomasia kutatua kadhia hiyo. Gazeti la Kizayuni la Haaretz limemnukuu kiongozi mmoja wa Kiyahudi ambaye hakutaka jina lake litajwe akisema kuwa, Obama alisema hayo siku ya Alkhamisi katika mkutano wake wa faragha na viongozi wa Mayahudi wa Marekani katika Ikulu ya nchi hiyo White House na kuongeza kuwa, yeye haungi mkono suala la kuivalia njuga kupindukia kadhia ya nyuklia ya Iran madhali bado kuna fursa ya kulitatua suala hilo kwa njia za kidiplomasia.
Mkutano huo umefanyika kwenye wakati huu wa kukaribia ziara ya Obama katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni. Ziara hiyo inatarajiwa kufanyika tarehe 20 mwezi huu wa Machi na itakuwa ya kwanza kufanywa na Obama tangu awe Rais wa Marekani mwaka 2009. Hata hivyo Obama amedai kwa mara nyingine kuwa, machaguo yote ya utatuzi wa kadhia ya nyuklia ya Iran yako mezani lakini siasa za hivi sasa za White House ni kuitatua kidiplomasia kadhia hiyo.
Marekani na waitifaki wake wanaeneza propaganda za uongo kuwa Iran inataka kumiliki silaha za nyuklia madai ambayo yanapingwa vikali na viongozi wa Tehran.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO