Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC imetoa wito wa kutumwa kamati ya jumuiya
hiyo nchini Myanmar kwa shabaha ya kushuhudia kwa karibu hali inayowakabili
Waislamu wa jamii ya Rohingya wa nchi hiyo. Taarifa ya mwisho ya mkutano wa
kamati ya mawasiliano ya OIC imeitaka serikali ya Myanmar kuruhusu kamati ya
mawaziri ya jumuiya hiyo kutumwa katika nchi hiyo. Akizungumza katika mkutano
huo, Profesa Ekmeleddin İhsanoğluKatibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa
Kiislamu OIC amesema kuwa, utumiaji mabavu unaofanywa dhidi ya Waislamu wa
Myanmar haukubaliki hata kidogo na kwamba, hiyo ni ishara ya utendaji mbaya wa
serikali ya nchi hiyo. Ni mwaka mmoja sasa ambapo OIC imekuwa ikitaka kutuma
kamati ya uchunguzi nchini Myanmar lakini bado haijafanikiwa hadi sasa. Katika
taarifa yake, Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC imeitaka Kamisheni ya Haki
za Binadamu ya Umoja wa Mataifa kutuma timu ya uchunguzi nchini Myanmar. Aidha
OIC imezitaka nchi jirani na Myanmar kama Bangladesh na Malaysia kusaidia
kutatua tatizo la Waislamu wa Rohingya wanaoandamwa na wimbi la mauaji
yanayofanywa na Mabudha wenye misimamo mikali wakishirikiana na askari wa jeshi
la serikali ya Myanmar.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO