Tuesday, April 16, 2013

WANNE WAUWAWA MACHAFUKO BAADA YA UCHAGUZI VENUZUELA

Watu wanne wameuawa kufuatia machafuko yaliyozuka baada ya uchaguzi wenye utata nchini Venezuela. Shirika la habari la kitaifa limesema kuwa watu wawili wameuawa katika jimbo la Miranda, ambalo linajumuisha maeneo ya Caracas, mmoja katika jimbo la Tachira katika mpaka na Colombia na mwingine katika jimbo la magharibi la Zulia. Upinzani awali uliitisha maandamano mengine leo kupinga kuidhinishwa mrithi wa rais wa zamani wa Venezuela Hugo Chavez, kama rais mpya. Maelfu ya wafuasi wa upinzani wamefurika katika barabara za mji mkuu Caracas jana wakati Tume ya Uchaguzi ilipotangaza kuwa kaimu rais Nicolas Maduro amemshinda mpinzani wake Henrique Capriles, ambaye amekataa kukubali matokeo , akidai kura zihesabiwe upya.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO