Serikali ya Zimbabwe imeamua kufuta ombi lake kwa Umoja wa Mataifa la kutaka isaidiwe kifedha katika kuendesha zoezi la uchaguzi mkuu ujao nchini humo.
Waziri wa Sheria wa Zimbabwe Patrick Chinamasa amesema, awali serikali ya Harare iliomba msaada wa fedha kutoka Umoja wa Mataifa za kudhamini uchaguzi mkuu, lakini tumeamua kuufuta kabisa mpango huo. Chinamasa ameongeza kuwa, kuna ulazima wa kutafutwa vyanzo vya ndani vya fedha vitakavyodhamini gharama za uchaguzi huo.
Hivi karibuni Tendai Biti Waziri wa Fedha wa Zimbabwe alisema kuwa, nchi yake inahitajia kiasi cha dola milioni 132 za kuendeshea uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwezi Juni mwaka huu.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO