Mwanajeshi wa jeshi la majini la Marekani amehukumiwa adhabu ya kifungo cha miaka 20 jela kwa kosa la kuchoma msikiti mmoja katika jimbo la Ohio nchini humo.
Jaji wa Mahakama ya Ohio amesema kuwa, Randy Linn mwanajeshi mstaafu amehukumiwa adhabu ya kifungo cha miaka 20 jela pamoja na kulipa fidia ya dola milioni moja na laki nne kutokana na uharibifu alioufanya kwenye msikiti huo. Linn ameiambia mahakama hiyo kwamba, anajutia kosa alilofanya kwa vile alilewa sana.
Mwanajeshi huyo mstaafu mwenye umri wa miaka 52 aliuteketeza kwa moto msikiti wa Kituo cha Kiislamu cha 'Great Toledo' katika jimbo la Ohio, ikiwa ni eti kulipiza kisasi cha kuuawa wanajeshi wa Kimarekani walioko nje ya nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO