Tuesday, April 09, 2013

NCHI 30 ZIKIONGOZWA NA MAREKANI KUFANYA MANUVA GHUBA YA UAJEMI


Msemaji wa jeshi la majini la Marekani amesema kuwa, zaidi ya nchi 30 zikiongozwa na Marekani zitafanya manuva makubwa ya kijeshi kwenye maji ya Ghuba yaUajemi katika kipindi cha wiki chache zijazo.  Msemaji wa jeshi la majini la Marekani amesema kuwa, mazoezi hayo ya kimataifa yatafanyika mwezi ujao katika eneo la maji ya Ghuba ya Uajemi.
Amesema kuwa, lengo la kufanyika manuva hayo yatakayoanza tarehe 6 hadi 30 ya mwezi Mei ni kufanya mazoezi ya kutegua na kukusanya mabomu ya kutegwa ardhini na operesheni ya kuzisindikiza meli za kibiashara katika eneo hilo. Hata hivyo, msemaji huyo alikataa kutaja nchi zinazoshiriki kwenye manuva hayo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO