Tuesday, April 16, 2013

SABRI AHIMIZA MSHIKAMANO WA UMMA WA KIISLAM DUNIANI


Khatibu wa Masjidul Aqswa amezitaka nchi za Kiislamu na Kiarabu kuimarisha mshikamano wa Kiislamu.
Sheikh Ikrima Said Sabri ameyasema hayo alipokutana na ujumbe wa Waislamu wanaoishi nchini Australia na kusisitiza kuwa, nchi za Kiislamu na za Kiarabu zinapasa kuimarisha mshikamano wa ulimwengu wa Kiislamu na Kiarabu na kuzidisha ushirikiano wao katika nyanja mbalimbali sanjari na kuchukua misimamo imara katika kukabiliana na changamoto na vitisho vinavyowakabili Waislamu katika maeneo mbalimbali duniani. Sheikh Sabri ameelezea hali halisi iliyopo Quds Tukufu na siasa za kibaguzi za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wakazi wa wananchi wa Palestina wanaoshi katika eneo hilo na kusisitiza kuwa, utawala wa Israel unataka kuuyahudisha mji huo mtakatifu. Ameongeza kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel unataka kubadilisha utambulisho wa kihistoria na kidini wa mji huo kwa maslahi ya Wazayuni.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO